●Kiasi cha gramu 8189.79 zakamatwa
●Leseni 65 za ununuzi mkubwa wa madini zatolewa
MBEYA-Mkoa wa kimadini Chunya mpaka kufikia Juni 7, 2024 umefanikiwa kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 34.9 katika mnyororo wa uchimbaji madini.


Akielezea kuhusu mwenendo wa utoaji leseni za ununuzi mdogo na mkubwa wa madini , Mhandisi Mayala amesema kuwa, idadi ya leseni 65 zimetolewa kwa wanunuzi wakubwa wa madini na leseni 315 za wanunuzi wadogo.
Akifafanua juu ya kuwaendeleza wachimbaji wadogo wilayani Chunya Mha.Mayala amesema kuwa tayari wametenga maeneo mbalimbali ikiwemo Makongolosi, Mawelo,Sagambi, Matundasi na Kasisi kwa ajili ya kurasimishwa kwa wachimbaji wadogo ili kukuza shughuli zao za uchimbaji.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali ameipongeza Ofisi ya Madini Wilayani Chunya kwa kufanya vizuri katika usimamizi mzuri wa shughuli zote zinazohusiana na sekta ya madini.

Ziara hii ya siku mbili wilayani Chunya Mahimbali ameambatana na watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Madini kwa lengo la kukagua shughuli mbalimbali za uchimbaji , uzalisha na uchenjuaji katika mnyororo mzima wa sekta ya madini.