BANGKOK-Asean Africa Minerals Investment Forum kwa kushirikiana na Tanzania-Thailand Chambers of Commerce chini ya uangalizi wa Consulate of Tanzania-Thailand wanaandaa kongamano la wadau mbalimbali wa madini mkakati (CRITICAL MINERALS) kuanzia Novemba 21 hadi 22,2024.

Kongamano hilo linatoa fursa ya wadau wote kuhudhuria kwa kujisajili kupitia tovuti maalum ya kongamano ambayo ni https://aseanafricaminerals.org/

Pia, Watanzania watakaoshiriki na kuongoza jopo katika mjadala na mazungumzo ni Kamishna wa Madini mstaafu, Dkt.Dalay Peter Kafumu (Speaker), Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazigira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka (Panelist) na Godwin Martin Hiza Nyelo (Panelist).