DAR-Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imetunukiwa tuzo kwa kuibuka mshindi wa pili miongoni mwa mamlaka za maji nchini katika utoaji wa taarifa kwa wananchi.


Aidha, mbali na tuzo hiyo, MWAUWASA imepokea Cheti cha kutambua jitihada za kipekee na mikakati bunifu ya mawasiliano inayotekeleza na ambayo imeleta mchango mkubwa katika Sekta ya Habari.
Kikao kazi hicho kimeshirikisha Maafisa Habari wa Serikali zaidi ya 500 kutoka Wizara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri mbalimbali kote Nchini.