Naibu Waziri Byabato ashiriki Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri EAC

ARUSHA-Mkutano wa 44 Wa Baraza la Kisekta La Mawaziri wa Viwanda, Biashara, Uwekezaji na Fedha (SCITIF) la Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika 31 Mei, 2024 jijini Arusha Tanzania. Mkutano huo ulitanguliwa na mikutano ya ngazi ya watalaam na Mkutano wa Makatibu Wakuu iliyofanyika kuanzia tarehe 27 hadi 30 Mei 2024.
Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo uliongozwa na Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb.), Waziri wa Fedha wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viongozi wengine walioshiriki ni Mhe. Sharif Sharif, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Stephen Byabato (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mhe. Exaud Kigahe, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.
Mkutano huo ulipokea na kujadili taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa 43 wa SCITIF, taarifa ya mashauriano ya Kibajeti wa Mawziri wa Fedha wa Jumuiya, taarifa ya Kamati za Forodha, Biashara, Uwekezaji, Viwango vya Afrika Mashariki na taarifa ya Mamlaka ya Ushindani ya Afrika Mashariki.
Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulieleza Serikali ya Kenya kufanya haraka kuajiri maafisa watakaokamilisha taratibu za kiforodha zinazotakiwa ili kuclear mizigo ya wafanyabiashara kutoka Tanzania wanaosafirisha mizigo yao kwenda nchini Kenya ili kuondoa usumbufu ambao umekuwepo kwa muda mrefu. Vilevile, Tanzania na Kenya zimekubaliana kutoza viwango sawa vilivyoidhinishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa magari yanayovuka mipaka ya nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news