MOROGORO-Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze amewaasa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukipigania chama chao kwa wivu mkubwa ili kulinda na kutekeleza malengo ya chama katika kuwahudumia wananchi na kuleta maendeleo kwa wananchi bila ubaguzi.
Mhe.Ridhiwani aliyabainisha hayo mkoani Morogoro wakati akihutubia Mkutano wa Kuwaaga Wanachama wa CCM Seneti ya vyuo na vyuo Vikuu uliofanyika katika chuo cha Mtakatifu Jordan mkoani humo.
"Hata kama ikifika siku chama hichi kinaona Ridhiwani hafai kuwa mwanachama wakaamua kunifukuza nitawapa kila kitu lakini kadi ya Chama cha Mapinduzi sitatoa kwasababu Chama cha Mapinduzi kipo moyoni mwangu na huu ndio msingi ambao mnatakiwa muwe nao,piganieni chama chenu msisubiri kukumbushwa jukumu hilo," alisisitiza Mhe. Ridhiwani.