OUT, VETA na FDC mbioni kuwanoa wafungwa nchini

DODOMA-Tume ya Haki Jinai imemweleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa,Jeshi la Magereza nchini lipo katika mazungumzo na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT),VETA na FDC ili kutoa elimu kwa wafungwa kuendana na Mitaala iliyopo uraiani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Sefue. Hafla ya upokeaji wa Taarifa hiyo imefanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 15 Juni, 2024.

Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameyasema hayo Juni 15, 2024 Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi Taarifa ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kwa Rais Dkt.Samia.


Amesema, elimu hiyo itawasaidia wafungwa wanapotoka magerezani kuwa na vyeti na ujuzi unaoendana na mahitaji

"Vile vile Jeshi la Magereza limeanza mazungumzo na taasisi kama vile Chuo Kikuu Huria, VETA na FDC ili kuwisanisha mitaala inayotolewa Magerezani na ile itolewayo uraiani ili iwe rahisi kwa wafungwa wanaomaliza adhabu zao kurejea uraiani wakiwa na vyeti vinavyotambulika kulingana na elimu na ujuzi walioupata wakiwa Magerezani."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news