Picha tatu bora zaidi za mwezi Mei,2024

TUNAPONGEZA jitihada hizi ambazo zinafanywa na Jeshi la Polisi Tanzania ambazo zinaendelea kudhirisha kuwa, ni jeshi rafiki kwa jamii, hivyo kondoa ile dhana iliyojengeka huko nyuma kuwa, askari hana urafiki na jamii hasa wanapofika katika vituo vya polisi.
Picha bora zaidi ya mwezi Mei, 2024 ni ya Mkuu wa Dawati la Elimu Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Rajabu Khatibu akimfunga kamba ya viatu mwanafunzi wa Shule ya Msingi St. Andrew Academy iliyopo jijini Arusha. Askari huyo pia aliwapa elimu kuhusu usalama barabarani na namna ya kutumia vivuko kuvuka salama.
Picha bora ya mwezi Mei ni Mkaguzi Kata wa Kata ya Butimba Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mkaguzi Mzaidizi wa Polisi A/Insp Dossantos Mwakyoma akimfundisha namna ya kusoma kitabu. Tukio hilo limetokea wakati mkaguzi huyo akiendelea na kampeni yake ya kutembelea nyumba kwa nyumba kutoa elimu.
Picha bora mwezi Mei, ni ya Mkaguzi wa Polisi Rehan Abuu ambaye ni Mkaguzi Kata ya Tandala Mei 31,2024 ametoa elimu katika shule ya chekechea Consolata Ikonda katika kata Lupalilo wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe na kuwaelimisha wanafunzi kusoma kwa bidii, kuwaheshimu walimu pamoja na wazazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news