ZANZIBAR-Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amekitaka Kigoda cha Taaluma cha Sheikh Abeid Amani Karume kutilia mkazo zaidi masuala ya kufanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya maendeleo nchini.
Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Juni 15,2024 alipozindua rasmi Kigoda cha Taaluma cha Sheikh Abeid Amani Karume katika ukumbi wa Dkt.Ali Mohamed Shein uliopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.
Ameeleza kuwa, Serikali itafanya juhudi za kuhakikisha malengo ya kigoda hicho yanafanikiwa ili kuleta tija za kihistoria, kitaaluma na kimaendeleo kwa ustawi wa jamii.
Rais Dkt.Mwinyi amesema,kigoda hicho kiwe ni jukwaa ambalo litaendeleza na kutunza tunu za taifa za Mapinduzi na Muungano ambazo zimetimiza miaka 60.
Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Profesa Egiland Pius Mihanjo kwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Kigoda hicho.
Viongozi mbalimbali wa Serikali,vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama wameshiriki wakiwemo Rais mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete,