Rais Dkt.Samia afanya uteuzi TBS,Kilolo, Misungwi na kutengua

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali na kutengua uteuzi mmoja.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Juni 22, 2024 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, viongozi walioteuliwa ni Dkt. Ashura Abdul Katunzi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kabla ya uteuzi, Dkt. Katunzi alikuwa Afisa Udhibiti Ubora Mkuu, Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Aidha, Dkt. Katunzi anachukua nafasi ya Dkt. Athuman Yusuf Ngenya ambaye amemaliza muda wake.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Hassan Juma Mnyika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo. Kabla ya uteuzi, Bw. Mnyika alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais-Ikulu. Bw.Mnyika anachukua nafasi ya Bw. Lain Ephraim Kamendu ambaye amestaafu.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Addo Missama kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi. Kabla ya uteuzi, Bw. Missama alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais-Ikulu. Bw. Missama anachukua nafasi ya Bw. Joseph Constantine Mafuru ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news