Rais Dkt.Samia akutana na mwanamuziki maarufu Korea aliyeimba Leopard of Kilimanjaro na Like Serengeti

SEOUL-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na mwanammuziki maarufu nchini Korea, Bw. Cho Yong-pil ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kutangaza vivutio vya utalii. Bw. Cho ambaye yupo katika fani ya mziki kwa zaidi ya miaka 50 anaelezwa kuwa ni mmoja wa wanamuziki nguli, wenye ushawishi mkubwa nchini Korea aliyeshinda tuzo mbalimbali kupitia kampuni ya YPC.
Bw. Cho ambaye ameimba nyimbo mbili kuhusu Tanzania, “Leopard of Kilimannjaro na Like Serengeti” alimweleza Rais Samia kuwa anaipenda Tanzania na anatamani kufika nchi hiyo kwa mara ya pili kabla hajaondoka hapa duniani. Rais Samia alimshukuru Bw. Cho kwa nyimbo zake hizo ambazo kutokana na umaarufu wake zimeitangaza Tanzania sio tu Korea bali duniani kote, na kumsihi arejee Tanzania ili atunge nyimbo kuhusu vivutio mbalimbali vya utalii na utamaduni.

Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Udaktari wa Falsafa wa Heshima (Honoris Causa) kwenye Sekta ya Anga na Rais wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Anga (Korean Aerospace University), Hee Young Hurr kupitia hafla iliyofanyika jijini Seoul leo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news