Rais Dkt.Samia asherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika na wajukuu



DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amesherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka.
Katika kuadhimisha siku hii, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema.

"Wasaa mzuri na wajukuu toka maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika hii leo. 

"Ndoto na matarajio ya watoto katika kila kona ya nchi yetu viendelee kutukumbusha jukumu la kila mmoja wetu katika kazi ya kujenga taifa bora kwa kuunda na kutekeleza sera sahihi, ikiwemo uwekezaji mkubwa tunaoendelea kuufanya katika sekta za elimu na afya.

"Tuendelee kuifanya kazi hii sambamba na ile ya kutunza amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu, kwani uhakika wa kesho yao ndio uhakika wa uimara, usalama na ustawi wa nchi yetu."
Pia,kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu, vilevile kuwapatia elimu na historia za kuwahimiza uzalendo kwa nchi yao tangu wakiwa wadogo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news