Rais Dkt.Samia ateua na kufanya uhamisho wa viongozi mbalimbali leo

UTEUZI WA NAIBU WAZIRI, NAIBU MAKATIBU WAKUU, MKUU WA WILAYA,WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI NA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU
 
Katika kuboresha utendaji kazi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
 
A) Uteuzi wa Naibu Waziri Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Mipango na Uwekezaji.
 
B) UTEUZI WA NAIBU MAKATIBU WAKUU
1. Bi. Felister Peter Mdemu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum anayeshughulikia masuala ya Jinsia na Wanawake. Kabla ya uteuzi, Bi. Mdemu alikuwa Msaidizi wa Rais, Maendeleo ya Jamii.
 
Aidha, Bw. Amon Anastaz Mpanju atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum anayeshughukia masuala ya Maendeleo ya Jamii na Makundi Maalum.
 
2. Bi. Zuhura Yunus Abdallah ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Kabla ya uteuzi, Bi. Abdallah alikuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.
 
C) UTEUZI NA UHAMISHO WA WAKUU WA WILAYA
1. Bw. Petro Magoti Itozya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe. Kabla ya uteuzi, Bw. Itozya alikuwa Msaidizi wa Rais, Siasa;
 
2. Bi. Fatma Almas Nyangasa amehamishwa kutoka Wilaya ya Kisarawe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa; na 3. Dkt. Hamis Athumani Mkanachi amehamishwa kutoka Wilaya ya Kondoa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo. Aidha, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bw. Elibariki Bajuta atapangiwa kazi nyingine.
 
D) UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA
1. Bw. Reuben Michael Chongolo amehamishwa kutoka Wilaya ya Songwe kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi; na 

2. Bw. Frank Mastara Sichwale amehamishwa kutoka Wilaya ya Mufindi kwenda kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe.
 
E) UTEUZI NA UHAMISHO WA WAKURUGENZI WATENDAJI WA HALMASHAURI
1. Bw. Mussa Abdul Kitungi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia;
 
2. Bi. Kalekwa Kasanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Kabla ya uteuzi, Bi. Kasanga alikuwa Afisa Sheria Mwandamizi, Tume ya Kurekebisha Sheria;
 
3. Bw. Shaaban Abdulrahman Mpendu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Mji wa Babati. Kabla ya uteuzi, Bw. Mpendu alikuwa Mhasibu Mkuu,  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro;
 
4. Bi. Sigilinda Modest Mdemu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Kabla ya uteuzi, Bi. Mdemu alikuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni;
 
5. Bi. Upendo Erick Mangali amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Babati kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga;
 
6. Bw. Kisena Magena Mabuba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma. Bw. Mabuba anachukua nafasi ya Bi. Mwantum Mgonja ambaye uteuzi wake umetenguliwa; na
 
7. Bi. Teresia Aloyce Irafay amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'.
 
F) UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA KUU

1. Bw. Nehemia Ernest Mandia ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi, Bw. Mandia alikuwa Msaidizi wa Rais, Sheria;

2. Bw. Projestus Rweyongeza Kahyoza ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi, Bw. Kahyoza alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi wa Masijala Kuu ya Mahakama Kuu, Dodoma; na
 
3. Bi. Mariam Mchomba Omary ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi, Bi. Omary alikuwa Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
 
Uapisho wa Naibu Waziri, Naibu Makatibu Wakuu na Majaji wa Mahakama Kuu utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news