Rais Dkt.Samia ateua viongozi mbalimbali akiwemo Msemaji Mkuu wa Serikali,Thobias Makoba

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka leo Juni 15,2024, viongozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-Amemteua Balozi Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda na Biashara. Kabla ya uteuzi, Balozi Dkt. Simbachawene alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Amemteua Bw. Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia utalii. Kabla ya uteuzi, Bw. Mabula alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais - Ikulu.

Aidha, CP. Benedict Wakulyamba atakuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anayeshughulikia Maliasili.

Amemteua Dkt. Habib Gallus Kambanga kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi, Dkt. Kambanga alikuwa Afisa Mwandamizi, Ofisi ya Rais – Ikulu.

Amemteua Bw. Thobias Makoba kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari -Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali. Kabla ya uteuzi, Bw. Makoba alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Bw. Makoba anachukua nafasi ya Bw. Mabhare Matinyi ambaye amepangiwa majukumu mengine.

Amemteua Bw. Ally Rajab Mketo kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukombe. Kabla ya uteuzi, Bw. Mketo alikuwa Afisa Tawala Mwandamizi, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukombe.

Bw. Mketo anachukua nafasi ya Bw. Onesmo Kisoka ambaye amestaafu.

Amemteua Jaji Dkt. Mary Caroline Levira kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto. Jaji Dkt. Levira ni Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Jaji Dkt. Levira anachukua nafasi ya Jaji Dkt. Gerald Ndika ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Leonard Douglas Akwilapo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA). Dkt. Akwilapo ni Katibu Mkuu Mstaafu na Mhadhiri Mwandamizi, Kikuu Kikuu cha Dodoma.

Dkt.Akwilapo anachukua nafasi ya Prof. Maurice Mbago ambaye amemaliza muda wake.

Amemteua Dkt. Noel Eusebius Mbonde kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo cha Ufundi Arusha. Dkt. Mbonde ni Mkurugenzi Mstafu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news