Rais Dkt.Samia awaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Juni 23,2024 Ikulu jijini Dar es Salaam amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Naibu Makatibu Wakuu kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2024. Viongozi hao walioapa ni: Dkt. John Stephen Simbachawene kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Bishara pamoja na Nkoba Eliezer Mabula kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii (Anayeshughulikia Utalii).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwaapisha Mabalozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 23 Juni, 2024. Viongozi hao walioapa ni: Balozi Selestine Gervas Kakele pamoja na Balozi Dkt. Habib Gallus Kambanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news