PRETORIA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Afrika Kusini usiku wa leo Juni 18,2024 ambapo kesho Juni 19,2024 anatarajiwa kuhudhuria hafla ya uapisho wa Rais mteule wa nchi hiyo, Cyril Ramaphosa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 18 Juni, 2024. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Waterkloof Pretoria nchini Afrika Kusini tarehe 18 Juni, 2024. Rais Samia anatarajia kuhudhuria hafla ya Uapisho wa Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa tarehe 19 Juni, 2024.