RC Chalamila azindua Kamati ya Uwekezaji Dar

DAR-Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila amezindua Kamati ya Uwekezaji mkoa wa Dar es Salaam, tukio la uzinduzi wa Kamati hiyo limefanyika katika ofisi za Kituo cha Uwekezaji (TIC), Kanda ya Mashariki.Akizungumza kwenye uzinduzi huo, leo Juni 4, 2024, RC Chalamila ameiagiza Kamati hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzingatia masuala ya uzalishaji, masoko, usafirishaji, kuhakikisha uwekezaji endelevu ili kufanikisha na kuleta tija kwenye sekta ya uwekezaji sanjari na biashara kwenye mkoa wa Dar es Salaam na taifa kwa ujumla.
Vile vile, RC Chalamila amesema Kamati hiyo imeundwa kwa sababu ya kuangalia maeneo yenye fursa kwenye sekta mbalimbali katika mkoa, amesema Kamati itaratibu mnyororo wa uwekezaji kwa Wawekezaji wanaotoka nje ya taifa na Wawekezaji wa ndani.

“Tunatarajia Kamati hii ya Uwekezaji itakuwa na utundu wa kuendeleza uwekezaji; mfano kuchochea uwekezaji zaidi kwa Wafanyabiashara, hapa Dar es Salaam tuna Wafanyabiashara wengi sana.
Pia, Kamati itatusaidia kuratibu mfumo wa masoko wa ndani na nje,” amesema RC Chalamila.

Aidha, amesema Kamati itashughulikia vikwazo vya Kikodi na masuala ya kisheria kwenye sekta ya uwekezaji pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali kufanikisha na kuleta uwekezaji wenye tija katika mkoa wa Dar es Salaam na taifa kwa ujumla.Kamati hiyo ya Uwekezaji ya mkoa inaundwa na Taasisi mbalimbali za Serikali 15 ikiwa na Wajumbe 19.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Dkt. Toba Nguvila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam na Katibu wa Kamati ni Fidelis Obanga, kutoka TIC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news