Serengeti yaishukuru TEA kwa miradi ya elimu

DODOMA-Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mkoani Mara imeitunuku cheti cha shukrani Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kutokana na kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu katika halmashauri hiyo.
Cheti hicho cha shukrani kimekabidhiwa katika ofisi za TEA jijini Dodoma leo Juni 3,2024 ambapo Diwani wa Kata ya Morotonga, Mhe. Musa Magasi Mseti alikikabidhi kwa niaba ya halmashauri.

Diwani huyo amesema, TEA imekua mdau mkubwa wa kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu katika halmashauri hiyo ambapo ameongeza Shule ya Sekondari Morotonga anakotoka imepata ufadhili wa ujenzi wa matundu 24 ya choo hatua ambayo itamaliza changamoto ya uhaba wa matundu ya vyoo.

Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA, Bw.Emmanuel Shirima amepokea cheti hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TEA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news