Serikali inathamini mchango wa matumizi ya nishati safi zote za kupikia-Mhandisi Rwebangila

📌 Yawatoa hofu sekta binafsi kudhani nishati safi ni gesi pekee

📌 Mchango wa gesi asilia nishati safi kuchangia asilimia10 miaka kumi ijayo

📌 Umoja wa Ulaya kuendelea kufadhili utekelezaji wa Nishati safi

DAR-Wizara ya Nishati imewatoa hofu wadau wa sekta binafsi kuwa, Serikali inathamini mchango wa matumizi yote ya nishati safi ya kupikia ikiwemo umeme, gesi na nishati zingine zote ambazo ni rafiki kwa mazingira na afya.
Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme, Mhandisi Styden Rwebangila wakati akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati,Mhandisi Felchesmi Mramba kwenye mjadala wa wadau wa sekta ya nishati waliokutana kujadili. 

Sambamba na kutathmini uelekeo wa Sekta ya Nishati ilipotoka, ilipo na inapoelekea baada ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2022/2023 ikiwemo changamoto zilizopo na namna ya kukabiliana nazo.

‘’Napenda kuwatoa hofu wadau wa sekta binafsi na Watanzania kuwa, nishati safi ya kupikia inajumuusha nishati zote na sio gesi pekee kama wengine wanavyodhani,’’amesema Kamishna Rwebangila.
Pia, amesema Wizara ya Nishat inathamini mchango unaotolewa na wadau wa maendeleo hususani Umoja wa Ulaya kwa kufadhili miradi mbalimbali kwenye sekta ya nishati hususani nishati safi ya kupikia na itaendelea kushirikiana nao kwenye upangaji wa mipango mkakati na uendelezaji wa sera.

Naye Meneja Mradi wa Nishati kutoka Umoja wa Ulaya, Massimiliano Pedretti amesema, Umoja wa Ulaya utaendelea kufadhili miradi ya nishati safi ya kupikia kupitia mfuko.maalumu wa nishati safi kulingana na mkakati na utekelezaji kufikia azma ya asilimia 80 ya watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034 kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema, ili Tanzania iweze kufikia azma yake ni lazima ichukue jitihada za makusudi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wauzaji wa mitungi ya gesi, watengenezaji wa wa majiko ya umeme ili kuchochea wananchi kutumia nishati safi ya kupikia kwa gharama nafuu na upatikanaji wa haraka.

"Tayari mradi wa mfuko maalumu wa nishati safi ya kupikia unafanya kazi na Wizara ya Nishati ili kuhakikisha taasisi kama magereza, shule, hospitali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wanafanya kazi kwa pamoja na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye maeneo yao."

Kwa upande wake Meneja Mradi wa Matumizi Nora ya Umeme kutoka Shirika la UNDP, Aaron Cunningham amesema kuwa,UNDP iliamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kwenye sekta ya nishati safi ya kupikia kwa kuhakikisha pia inaanzisha programu hiyo.

Ni ili kuwe na matumizi bora ya nishati ya umeme kwenye vifaa vitakavyotumiwa na wadau na kuongeza kuwa tayari wameshaainisha viwango vtakavyotumiwa kwenye bidhaa aina tano kama vipoza umeme,jokofu, televisheni, feni,na majiko ya umeme ili vitumie umeme kidogo.
Amesema,mradi huu unatekelezwa kwa pamoja na Wizara ya Nishati tangu walipoanzisha mwaka 2022 na wamekuwa bega kwa bega na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili viwango hivyo vitoe unafuu wa matumizi ya umeme kwenye vifaa hivyo.

Umoja wa Ulaya umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa kwenye bajeti na miradi ya maendeleo hususani miradi ya umeme.

Mkutano huo ulihudhuriwa na taasisi zilizoko chini ya wizara ikiwemo REA,EWURA,TPDC,PURA, TANESCO pamoja na wadau wa maendeleo na sekta binafsi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news