*Azindua Sera ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya
MWANZA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameziagiza Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu zikae pamoja na Wizara ya Fedha na kuandaa mpango wa kitaifa wa kuwawezesha kujikimu vijana wanaoachana na matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Amesema, kutekelezwa kwa agizo hilo kutawawezesha vijana hao kupata mitaji ambayo itawawezesha kushiriki kwenye shughuli za ujasiriamali ambazo zitawasaidia kukuza kipato chao.

Ametoa agizo hilo leo Juni 30, 2024 wakati akizungumza na wananchi na wadau mbalimbali walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyamagana, jijini Mwanza.
“Wako wengine wanaohitaji kilimo, Wizara ya Kilimo itoe utaratibu; wapo wanaohitaji ufundi, Wizara ya Elimu itoe utaratibu, lengo ni kuhakikisha vijana hawa wakitoka huko wanakuwa na shughuli ya kufanya ili kujikimu.”

“Niwahimize wananchi wote wakiwemo wazazi, walezi, viongozi wa dini na taasisi za afya, tuendelee kupiga vita dawa za kulevya kwa vitendo na kuhakikisha jamii yetu haijihusishi na biashara, haifanyi uzalishaji wala matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo kutokomeza kilimo cha bangi na mirungi,” amesisitiza.

Pia ametoa pongezi kwa viongozi wa taasisi hiyo kwa jitihada zilizofikiwa kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ambapo hadi sasa Serikali imefanikiwa kujenga zaidi ya vituo 16 vinavyohudumia waraibu 16,460 kutoka vituo vitatu vilivyokuwepo mwaka 2017.

"Hivyo, napenda kuwahimiza sote tujitolee kikamilifu kutekeleza Sera hii ya Taifa. Tuwe walinzi wa vijana wetu na tukishirikiana, tunaweza kufanikisha lengo la kuwa na jamii salama na yenye afya njema.”

Amesema mashine hiyo iliyopo kwenye maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepata ithibati ya Umoja wa Mataifa na ina uwezo wa kuchukua zaidi ya sampuli 250 kwa saa 24.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)
Ofisi ya Waziri Mkuu