Serikali yahitimisha majadiliano mikataba minne utozaji kodi mara mbili Kimataifa

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Fedha, Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba amesema, kwa mwaka 2023/24 wizara yake imehitimisha majadiliano ya mikataba minne ya utozaji kodi mara mbili kati ya Tanzania na nchi washirika.

Nchi hizo ni Jamhuri ya Czech, Jamhuri ya Kisultani ya Oman, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mkataba wa pamoja wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo hatua za kusainiwa kwa mikataba hiyo zinaendelea.
Ameyasema hayo leo Juni 4, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Fedha kwa mwaka 2024/2025.

"Aidha, mkataba wa utozaji kodi mara mbili kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu umesainiwa na utekelezaji wake utaanza Januari 2025.

"Manufaa ya kuhitimishwa na kusainiwa kwa mikataba hiyo ni kuondoa vikwazo vya kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na nchi husika, kuvutia mitaji kutoka nje,

"Kuongezeka kwa fursa za ajira, kupanua wigo wa fursa za kibiashara na soko la malighafi, bidhaa na huduma zinazozalishwa na wawekezaji wa ndani."

Waziri Dkt.Nchemba amesema,hatua iliyofikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 aya ya 46 (b-d).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news