Serikali yaidhinisha fungu ujenzi Daraja la Kiloka lililosombwa na maji

MOROGORO-Serikali imeshaidhininisha kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kiloka linaounganisha kijiji cha Kiloka na vijiji jirani ambalo lilisombwa na maji ya mvua zilizonyesha mwanzoni mwa mwaka huu nchini.Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua ujenzi wa miindombinu ya barabara na madaraja inayosimamiwa na Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) mkoani Morogoro.
Mhandisi Mativila amesema,Serikali imetoa fedha hizo kuweza kurejesha mawasiliano katika vijiji hivyo ili wananchi waweze kuendelea kupata huduma za kijamii pamoja na zile za kiuchumi.

“Serikali imejikita kwenye ukarabati wa miundombinu ya barabara na madaraja yaliyoathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua za Elnino,hivyo fedha hizi zitaenda kurejesha mawasiliano kwa kujenga daraja hili la Kiloka na vijiji vya jirani”.
Hata hivyo, Mhandisi Mativila aliitaka TARURA kuendelea kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo ili kuwawezesha wananchi kuweza kuendelea na shughuli zao za kiuchumi kama ilivyokuwa awali.

Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro Mhandisi Mohamed Muanda amesema wanaishukuru serikali kwa kuwapati fedha hizo ambazo zitaenda kurejesha mawasilino ya vijiji vya jirani kupitia daraja la Kiloka.
Amesema, fedha hizo zitaenda kujenga daraja hilo lenye urefu wa mita 12 na kuliwekea kingo za mto pamoja na ukarabati wa tuta la barabara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news