Serikali yaanza kuchunguza Mifumo ya Viwanja vya Ndege

ZANZIBAR-Serikali imeanza uchunguzi maalumu wa kubaini mapungufu mbalimbali katika viwanja vyote vya ndege nchini ili kubaini changamoto hizo na kuweza kuzifanyia kazi ikiwemo mapungufu ya kimfumo,utendaji na upungufu wa miundombinu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiiongoza Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuwasili eneo la Mradi wa Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa ziara ya kamati hiyo Visiwani Zanzibar.Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,Vicent Mbogo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Ni ili kuweza kuboresha sehemu husika lengo ikiwa kurahisisha uingiaji na utokaji wa wageni ikiwemo watalii wanoukuja nchini kwa shughuli za utalii ambao uiingizia nchi kiasi kikubwa cha fedha.

Sambamba na kudhibiti uhalifu unaotokea katika viwanja vya ndege ikiwemo utoroshaji wa vito vya thamani,mnyororo wa upitishaji na uingiaji wa dawa za kulevya na uingiaji nchini kwa wageni bila kufuata sheria na taratibu za kiuhamiaji.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni wakati wa Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama ambapo kamati hiyo ilitembelea na Kukagua Mifumo ya Uhamiaji Mtandao katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Ujenzi wa Chuo cha Uhamiaji Kitogani na Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji mkoa wa Mjini Magharibi Mazizini.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo Uhamiaji Zanzibar, Mrakibu Msaidizi, Mvita Yussuf akitoa maelezo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama, Vicent Mbogo(kushoto) jinsi Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi unavyoendelea.Katikati ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Hassan Ali Hassan.Picha na Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Mbali ya kazi nzuri ambazo zinafanywa na Uhamiaji lakini kuna maeneo tunataka kupeleka nguvu zaidi hasa maeneo ambayo kwanza ni sura ya nchi.

"Malango makuu ya kuingilia kama hapa tulipo katika maeneo ya Viwanja vya Ndege,mtu akija Tanzania sura ya nchi inamuonyesha anapopokelewa katika viwanja vya ndege,haipendezi mgeni akija hapa nchini apange mstari mrefu,mara viyoyozi havifanyi kazi ndio maana serikali kuna uchunguzi maalumu tunafanya ili kuweza kubaini mapungufu hayo na kuyafanyia kazi katika Viwanja vyote vya ndege nchini,"alisema Waziri Masauni.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Vicent Mbogo akimuuliza maswali Mkuu wa Kitengo cha Majengo, Uhamiaji Zanzibar, Mrakibu Msaidizi, Mvita Yussuf(kulia) baada ya kukagua Ujenzi wa Ujenzi wa Ofisi ya Uhamiaji ya Mkoa wa Mjini Magharibi wakati wa ziara ya kamati hiyo Visiwani Zanzibar.Katikati ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan.Picha na Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Akizungumza katika ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama,Vicent Mbogo amesema ni muhimu mapungufu hayo katika viwanja vya ndege yakafanyiwa kazi huku akisifu juhudi za serikali zote mbili katika kuiletea Zanzibar maendeleo ambapo alisema Zanzibar ni nchi ya utalii ni vyema huduma malango yan chi zikaboreshwa.

"Zanzibar imeendelea kwa kasi kubwa pamoja na maendeleo haya ya miundombinu katika uwanja wa ndege ambapo sasa yanasomana na kule Tanzania Bara tumeona maendeleo yanafanyika katika viwanja vyetu ambavyo ndio maingilio ya watalii ambao wanatuletea fedha nyingi hapa nchini,napenda kwapongeza Marais wetu,Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ali Mwinyi wanafanya kazi kubwa sana kuiletea nchi yetu maendeleo,"alisema Mbogo.
Afisa Mfawidhi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume,Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji,Abdul Rahman Khamis Juma akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama jinsi shughuli za uhamiaji ikiwepo uingiaji na utokaji wa raia na wageni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.Wakwanza kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni na wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati,Vicent Mbogo.Picha na Wizara wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Naye Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan alitaja jinsi miradi ya maendeleo ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 ilivyokamilika ikiwemo Ujenzi wa Ofisi ya Uhmiaji mkoa wa Mjini Magharibi,Mkoa wa Kusini Pemba,Ukarabati wa Ofisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar,Ukarabati wa Nyumba ya Makazi ya Askari Ndugu Kitu Chake Chake Pemba na Ukarabati wa Nyumba Mbili za Makaazi ya Askari Mtemani Wete na Pemba ambapo imekamilika kwa asilimia mia moja huku gharama yake ikiwa ni kiasi cha Shilingi Bilioni 1.9.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news