Serikali yawataka wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba ya fedha

NA CHEDAWIE MSUYA
WF

WANANCHI wametakiwa kukopa mikopo yenye faida kwenye taasisi au mtu binafsi ambaye ana leseni iliyotolewa na Benki Kuu ya Tanzania ili kuwa na uhakika wa mkopo na kuondoa changamoto kwa wananchi hao.
Baadhi ya Wajasiriamali wakisikiliza semina kuhusu Elimu ya fedha na uwekezaji yaliyofanyika katika soko la Mabamba, Wilaya ya Kibondo.

Wito huo umetolewa katika Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma na Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha Bw. Stanley Kibakaya, wakati wa zoezi la kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi mbalimbali katika Mkoa wa Kigoma.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya, akitoa semina ya mafunzo ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji kwa wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho kilichopo kata ya Kibondo mkoani Kigoma.

“Hakikisha unapokwenda kukopa, mkopeshaji awe na leseni kwa kuwa mtoa huduma huyo atakuwa amekidhi vigezo na masharti vilivyowekwa na mamlaka husika”, alisema Bw. Kibakaya.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha Bi. Grace Samwel, akitoa elimu ya fedha kwa Wajasiriamali katika soko la Mabamba, Wilaya ya Kibondo.

Aidha, aliwahimiza wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kuweka akiba ili kuweza kutambua mapato wanayo yapata kupitia biashara zao.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha, Bi. Grace Samwel akitoa semina kuhusu Elimu ya Fedha na Uwekezaji kwa wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo mkoani Kigoma.

Alisema kuwa wakitunza fedha lazima wawe na malengo ili akiba hiyo iwe na faida na pia ni vema wahifadhi fedha kwenye akaunti za Benki au kwenye simu, sehemu ambazo ni salama ili kuepuka hasara au upotevu.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo wakisikiliza semina ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo hicho, Mkoani Kigoma.

Kuhusu uwekezaji, Bw. Kibakaya, alisema kuwa jambo hilo si kwa ajili ya watu wenye kampuni kubwa pekee bali hata mwananchi wa kawaida anaweza kuwekeza kupitia biashara ndogondogo anazozifanya.
Diwani wa Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo, Mhe. Shedrack Chongela, akizungumza na wananchi kuhusu mafunzo ya Elimu ya Fedha na Uwekezaji yaliyofanyika katika Soko la Mabamba Wilaya ya Kibondo, Kigoma.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabamba, Wilayani Kibondo Bw. Shedrack Chongela, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa elimu waliyoitoa kwa wananchi hao huku akiwakumbusha wananchi wanapokwenda kuchukuwa mikopo waende maeneo yenye kukidhi vigezo.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha - Wizara ya Fedha, Bw.Stanley Kibakaya, akitoa elimu ya fedha kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afisa Tabibu Kibondo, mkoani Kigoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WF, Kigoma).

Naye Mkazi wa Kijiji cha Mabamba, Wilaya ya Kibondo, Bi. Felister Kazombe, alisema kuwa semina hiyo ni muhimu kwa jamii yao kwa kuwa imetoa mwongozo mzuri kuhusu masuala ya fedha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news