GEITA-Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo imara na inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati.



Amesema hayo leo Juni 2, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Katoro uliopo mkoani Geita.