Simiyu watakiwa kutumia Elimu ya Fedha kukuza uchumi

NA ASIA SINGANO
WF

WANANCHI wa Mkoa wa Simiyu wametakiwa kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata elimu ya fedha kutoka kwa wataalamu kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kutumia elimu watakayoipata kukuza uchumi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Kenani Kihongosi (watatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo (wa tatu kushoto) pamoja na Timu ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha, wakiongozwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Bi. Elizabeth Mnzava (wa pili kulia), Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Mwile Kauzeni (wa kwanza kulia), Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha Mkoa wa Simiyu, Bw. Mustapha Ayubu (wa kwanza kushoto) na Afisa mwingine kutoka Wizara ya Fedha Bi. Glory Kenedy (wapili kushoto), baada ya Timu hiyo kumtembelea Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Kenani Kihongosi, Ofisini kwake kabla ya kuelekea Wilayani Itilima kutoa elimu ya fedha kwa wananchi.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Kenani Kihongosi, Ofisini kwake, alipotembelewa na Timu ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kabla ya wataalamu hao kuelekea Wilayani Itilima Mkoani Simiyu kutoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara, wajasiriamali na wananchi wa Wilaya hiyo.
Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akizungumza kwa niaba ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha (hawapo pichani), kutoka Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), baada ya wataalamu hao kufika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Bw. Kenani Kihongosi (kushoto), kabla ya kuelekea wilayani Itilima Mkoani Simiyu kutoa elimu ya fedha kwa wananchi.

‘’Niwasisitize na kuwaomba wananchi wetu wapokee mpango huu kwa sababau ni mpango utakaowasaidia wao kujua matumizi sahihi ya fedha zao na namna bora ya kuchukua, kutumia mikopo na kufahamu mikataba namna gani mikopo wanayochukua inaweza kuwanufaisha katika maisha yao,"amesema Bw. Kihongosi.
Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Kenani Kihongosi, nyenzo ya kufundishia elimu ya fedha, mara baada ya kufika ofisini kwake kabla ya kelekea Wilayani Itilima Mkoani Simiyu kutoa elimu ya fedha kwa wajasiriamali na wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kuweka akiba, uwekezaji sehemu sahihi, umuhimu wa bima, na namna bora ya kuandaa maisha ya kustaafu na ya uzeeni kwa ujumla.

Aliongeza kuwa kauli mbiu ya kampeni hiyo isemayo ‘’Elimu ya Fedha ni Msingi wa Maendeleo ya Kiuchumi’’ ni muafaka kwa kuwa maendeleo ya kiuchumi lazima yatokane na mipango thabiti na mikakati bora ya elimu ya matumizi sahihi ya fedha hasa kwa wananchi.
Bw. Kihongosi, aliipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa mpango wa maendeleo ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya fedha nchi nzima na kuufikia Mkoa wake kutokana na umuhimu wa elimu hiyo katika kukuza uchumi wa nchi.
Baadhi ya wajasiriamali na wananchi wa Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha (Vikoba), utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha ili kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya fedha kwa njia rahisi.

‘’Niwapongeze, Wizara ya Fedha kwa kuja na mpango huu mkakati mzuri kabisa wa kuelimisha wananchi wetu kwa sababu ni imani yetu wananchi wakipata uelewa kuhusu masuala ya kifedha watafanya mambo mazuri yatayowasaidia kuleta tija kiuchumi,’’alisema Bw. kihongosi.
Picha za matukio mbali mbali ya mafunzo ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, elimu hiyo ya fedha ilianza kutolewa maeneo ya mijini kupitia maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha kwa Mikoa ya Dar Es Salaam, Mwanza na Arusha, ambapo kwa sasa programu hiyo imejikita kuwafikia wananchi wote kwa lengo la kuwaongezea uelewa wa masuala ya Fedha ili waweze kufanya maamuzi sahihi katika mahitaji na matumizi ya huduma za fedha.

Akitoa ufafanuzi kuhusu sifa za kukopa baada ya mmoja ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha katika Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bw. Alex Elias kutaka kufahamu kuhusu suala la kukosa mkopo kutokana na umri kuwa mkubwa, Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Mwile Kauzeni, alisema suala la mikopo ni haki ya watu wote wenye uwezo wa kulipa mikopo hiyo isipokuwa watoto.
Katibu Tawala Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Bi. Mwanana Msumi (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu wa kutoa elimu ya fedha wakiongozwa na Afisa Usimamizi wa Fedha kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Bi. Elizabeth Mnzava (watatu kushoto), Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Mwile Kauzeni (watatu kulia), na maafisa wengine wa Serikali, walipowasili wilayani Itilima kabla ya kuanza kutoa elimu ya fedha kwa wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo.

‘’Kuna taasisi moja inayoangalia taarifa za watu wote wanaokopa katika taasisi zote Tanzania, inaitwa Credit Info, hawa watu kila mtoa huduma ameambiwa apeleke majina ya watu wake ambao wamekopa sasa jina lako likipelekwa kule wanaona kwamba kumbe fulani amekopa mahali pengi, je anakopesheka tena? lakini ili mtu aweze kukopa ni yeye mwenyewe kuwa na uwezo wa kuingiza kiasi gani kila mwezi,” alifafanua Bi. Kauzeni.
Afisa Mkuu Mwandamizi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bi. Mwile Kauzeni, akimwelezea Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Faraja Msigwa (hayupo pichani) lengo la Afisa huyo Mwandamizi kuambatana na Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha (hawapo pichani) kutoa elimu ya fedha, baada ya kufika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Wilaya ya Itilima kabla ya kuelekea eneo lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapa wananchi wa Wilaya hiyo elimu ya fedha. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha-Simiyu).

Naye Afisa Usimamizi wa Fedha, kutoka Wizara ya Fedha, Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha, Bi. Elizabeth Mnzava, alisema Timu hiyo ya wataalamu wa kutoa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha inaendelea kutoa elimu hiyo katika Wilaya za Mkoa wa Simiyu ikiwemo Busega na Meatu ambapo baada ya kukamilisha Wilaya hizo wataalamu hao wataelekea Mkoani Shinyanga kutoa elimu ya fedha kwa wananchi wa mkoa wa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news