Tanzania, Global Fund kukuza ushirikiano kutokomeza Ukimwi, kifua kikuu na malaria

GENEVA-Serikali ya Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania na Taasisi ya Global Fund kuendelea kushirikiana ili kutekeleza vipaumbele vya Serikali vinavyolenga kutokomeza magonjwa ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria. Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Mei 30, 2024 kwenye kikao na Mkuu wa Usimamizi wa Ruzuku wa Global Fund Bw. Mark Eldon-Edington kilichofanyika pembezoni mwa Mkutano wa 77 wa Shirika la Afya Dunia (WHO) jijini Geneva nchini Uswisi.
"Nakushukuru sana Bw. Eldon-Edington kwa kuwa Taasisi yako ya Global Fund imechangia kwa kiasi kukubwa nchini Tanzania kupunguza vifo vitokanavyo na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria na pia kuimarisha mifumo ya afya iliyo stahimilivu na endelevu,"amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema kwa sasa changamoto kubwa iliyopo katika Sekta ya Afya ni kutomudu ugharimiaji wa baadhi ya vipaumbele vya kukabiliana na magonjwa pamoja ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaleta athari kubwa katika kutoa huduma za afya.
Kwa upande wake, Bw. Eldon-Edington ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika kupunguza maambukizi mapya na vifo vitokanavyo na UKIMWI.

"Global Fund itaendelea kutoa kipaumbele kwa Tanzania katika kutoa msaada ili kuimarisha mifumo ya afya itakayowezesha uendelevu katika mwitikio wa kutokomeza magonjwa haya,"amesema Bw. Eldon-Edington

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news