Tanzania, Guinea-Bissau zasaini Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau,Mheshimiwa Umaro Sissoco Embaló leo Juni 22,2024 wameshuhudia mawaziri wa Mambo ya Nje wakitia saini Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Umaro Sissoco Embaló, wakati wakishuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya nchi mbili, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 22 Juni, 2024. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akitia saini kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira akitia saini kwa upande wa nchi yake.
Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba baada ya kutia saini mkataba huo kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa na Jamii wa Jamhuri ya Guinea-Bissau Mhe. Carlos Pinto Pereira ambaye ametia saini kwa upande wa nchi yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló leo Juni 22,2024 Ikulu jijini Dar es Salaam baada ya mawaziri wa Mambo ya Nje kusaini Mkataba wa Muongozo wa Ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news