Tanzania ina umeme wa kutosha kufanya shughuli za kiuchumi-Dkt.Biteko

📌Asisitiza hakuna mgawo wa umeme

📌Amshukuru Rais Samia kuiimarisha Sekta ya Nishati

GEITA-Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa, kwa sasa nchi ina umeme wa kutosha kuwawezesha Watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi.Dkt. Biteko amesema hayo leo Juni 9, 2024 wakati alipoungana na Waumini wa Kanisa la AIC Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita kwenye ibada ya Jumapili.
"Nashukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia ameweka mipango madhubuti kwenye sekta yetu ya nishati ambayo sasa imepelekea tuwe na umeme wa kutosha na hatuna mgawo wa umeme,"amesema Dkt.Biteko.

Ameongeza kuwa, miezi michache iliyopita, tatizo la mgawo wa umeme lilikuwa likimkosesha amani, lakini kwa juhudi za viongozi Wakuu wa Serikali, Wizara na TANESCO limefikia tamati.
Kutokana na uwepo wa umeme mwingi wa kutosha, Dkt. Biteko amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo na kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi ya kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news