Tanzania kupokea zaidi ya shilingi trilioni 6 kutoka Jamhuri ya Korea

SEOUL-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais Yoon Suk Yeol wa Jamhuri ya Korea wameshuhudia utiaji saini wa mkataba mmoja, hati za makubaliano (MOU) mbili na tamko la pamoja la kuanzisha Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi (EPA).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi na Fedha (Jamhuri ya Korea) Choi Sang Mok wakisaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya Tanzania na Korea kuhusu Mkopo unaotolewa na Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea (Economic Development Cooperation Fund-EDCF). Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Mkataba huu utaiwezesha Tanzania kupokea mkopo kutoka Korea wa kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 2.5 kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2024 hadi 2028.

Ni kwa ajili ya miradi ya miundombinu ya maendeleo zinatolewa chini ya Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Uchumi wa Serikali ya Korea (EDCF).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakibadilishana Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Madini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Jamhuri ya Korea kuhusu Ushirikiano katika Madini ya Kimkakati. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.

Ili kufungua milango zaidi ya ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi, Tanzania na Korea zimesaini pia mkataba wa EPA utakaowezesha kuufanya uhusiano kuwa wa kimkakati hususani katika Nyanja za Biashara, Uwekezaji, Viwanda, Usafirishaji n.k.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba pamoja na Waziri wa Uvuvi na masuala ya Bahari kutoka Jamhuri ya Korea Kang Do-Hyung wakisaini Hati baina ya nchi mbili kuhusu Ushirikiano katika maendeleo ya Uchumi wa Buluu. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Tanzania ni miongoni mwa nchi tatu tu barani Afrika ambazo zitafanya majadiliano hayo yatakayozaa Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Korea, nchi nyingine ni Morocco na Kenya.

Hati za makubaliano zilizotia saini leo Juni 2,2024 ni pamoja na Ushirikiano katika Uchumi wa Buluu ambapo Tanzania itashirikiana na Korea Kusini katika maeneo ya uvuvi, viwanda vya kuchakata mazao ya bahari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Korea Mhe. Yoon Suk Yeol wakati wakishuhudia Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji pamoja na Waziri wa Biashara wa Korea Inkyo Cheong wakisaini Tamko la Pamoja kuhusu Uanzishwaji wa Majadiliano juu ya Mkataba wa Ushirikiano Kiuchumi. Hafla ya utiaji saini imefanyika katika Ikulu nchini humo tarehe 02 Juni, 2024.
Pia, ujenzi wa bandari za uvuvi, teknolojia na tafiti za masuala ya bahari, pia Wizara ya Madini ya Tanzania na Wizara ya Biashara, Viwanda na Nishati ya Korea Kusini zimetia saini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano katika Madini ya Kimkakati.

Tanzania na Korea Kusini zitashirikiana katika utafiti, uwekezaji, uchimbaji na kujenga uwezo wa kuongeza thamani ya madini ya kimkakati chini Tanzania. Madini hayo ni Nickel, Lithium na Kinywe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news