Tanzania na Pakistan zasaini Muhtasari wa Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa

DAR-Kaimu Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Marcus Mbilinyi amefanya mazungumzo na Balozi wa Pakistan nchini Tanzania, Mhe. Siraj Ahmed Khan jijini Dar es Salaam leo Juni 24, 2024.Wakati wa mazungumzo hayo viongozi hao walisaini Muhtasari wa Makubaliano ya Mashauriano ya Kisiasa kati ya Tanzania na Pakistan (Agreed Minutes of the Bilateral Political Consultations-BPC).
Makubaliano hayo ambayo majadiliano yake yalifanyika mwezi Machi 2024 yaligusia ushirikiano kwenye biashara; uwekezaji; elimu; sayansi, teknolojia; mafunzo ya kujengeana uwezo; ulinzi, usalama; utamaduni na masuala ya kikonseli.
Kwa ujumla makubaliano hayo yalilenga kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kwa faida na mustakabali bora wa nchi hizi mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news