Tanzania yashiriki kikamilifu Mkutano wa 47 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma wa SADC

MAPUTO-Mkutano wa 47 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa Ngazi ya Wataalam unafanyika jijini Maputo, Msumbiji tarehe 04 hadi 07 Juni, 2024.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Juni 5,2024 na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Maputo,Msumbiji.

Mkutano huo unajadili masuala mbalimbali kuhusu Makubaliano ya Biashara ya Huduma kwa Nchi Wanachama wa SADC yakiwemo; Mapitio ya Taarifa ya Mkutano wa 46 wa Jukwaa la Majadiliano ya Biashara ya Huduma uliofanyika tarehe 09 -11 Novemba, 2023 jijini Cape Town, Afrika Kusini.

Pia, kuandaa Mkakati wa Biashara ya Huduma katika Jumuiya ya SADC na Mpango Kazi wake kwa Kipindi cha Miaka Mitano (2025-2029).

Vile vile, kupokea Taarifa za Hatua za Utekelezaji kutoka Nchi Wanachama kuhusu Ufunguaji wa Sekta za Biashara ya Huduma za Awamu ya Pili.
Sambamba na kuandaa Taarifa ya Masuala ya Biashara ya Huduma ambayo itajumuishwa kama mojawapo ya Agenda za Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa Biashara wa Jumuiya ya SADC.

Ujumbe wa Tanzania kweye Mkutano huo, unaongozwa na Bi. Angelina Bwana, Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news