TAWA yatwaa tuzo na vyeti Tanga Trade Fair

NA BEATUS MAGANJA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imepokea tuzo ya mshindi wa pili wa jumla kwenye maonesho ya 11 ya utalii na biashara maarufu Tanga Trade Fair.
Ni yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara mkoani Tanga kuanzia Mei 28, 2024 mpaka Juni 6, 2024.
Sambamba na tuzo hiyo, TAWA pia imetunukiwa vyeti vitatu kwa ushindi na pongezi kwa kushiriki na kufanikisha maonesho hayo.

Tuzo na vyeti hivyo vilitolewa Juni 06, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dkt. Batilda Buriani ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuhitimisha maonesho hayo kwa Mwaka 2024 ambapo taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zilishiriki.
Licha ya kujikusanyia tuzo na vyeti mbalimbali vya pongezi, TAWA pia imepongezwa kwa kufanikisha uwepo wa wanyamapori hai ambao walikuwa kivutio kikubwa na hamasa ya watu wengi kuhudhuria na kushiriki katika maonesho hayo.

TAWA imeshiriki kikamilifu maonesho hayo ya biashara na utalii yaliyokuwa na kauli mbiu "Kufungua fursa za kiuchumi kupitia ushirikiano wa Sekta za Umma na Binafsi" ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukuza na kutangaza Utalii wa nchi yetu.

Aidha, TAWA imetumia maonesho hayo kunadi fursa mbalimbali za utalii na uwekezaji zilizosheheni katika taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria katika maonesho hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news