TIRA ndani ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2024 Dodoma

DODOMA-Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2024 yanayofanyika jijini Dodoma.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “KUWEZESHA KWA UTUMISHI WA UMMA ULIOJIKITA KWA UMMA WA AFRIKA YA KARNE YA 21 ILIYOJUMUISHI NA INAYOSTAWI; NI SAFARI YA MAFUNZO NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA” ambapo wizara na taasisi mbalimbali za Serikali zinaonesha na kutoa huduma mbalimbali za serikali moja kwa moja.
Maadhimisho haya yanasindikizwa na Maonesho yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali Park ambapo ufunguzi rasmi wa maonesho hayo ni tarehe 19 Juni 2024. Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 16 Juni, 2024 yatamalizika tarehe 23 Juni 2024.

Kupitia maonesho haya, TIRA inawakaribisha wakazi wa Dodoma na wote walio mikoa ya jirani kutembelea banda lake ambapo kuna wataalamu mbalimbali wanaotoa maelezo na taarifa mbalimbali zinazohusu bima.
Baadhi ya mambo muhimu ambayo wananchi wanaweza kuyapata kwenye banda la TIRA ni pamoja na; Kupata elimu ya Bima ambapo wataelimishwa kuhusu aina mbalimbali za bima, umuhimu wake, na jinsi zinavyoweza kusaidia katika kupunguza athari za majanga na ajali mbalimbali.

Pia, huduma za ushauri ambapo wataalamu wa TIRA watakuwa tayari kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala ya bima, ikiwa ni pamoja na jinsi ya kuchagua bima bora inayokidhi mahitaji ya mtu binafsi au biashara.

Vile vile maonesho ya bidhaa za bima yatakayowapa wananchi fursa ya kuuliza maswali na kupata maelezo zaidi na kusajili wa malalamiko kwa wale wenye malalamiko au changamoto zinazohusiana na huduma za bima pamoja na kupata ushauri na msaada wa kitaalamu.
Hii ni fursa muhimu kwa wananchi na wadau wa bima nchini Tanzania kujifunza zaidi kuhusu huduma na faida za bima.

Ushiriki katika maonesho haya ni muhimu hivyo wananchi wanahimizwa kutembelea banda la TIRA kwa wingi ili kupata maarifa yatakayowasaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu bima.

Kuwa na ufahamu sahihi kuhusu bima kunatoa fursa ya kulinda mali na maisha dhidi ya hatari mbalimbali.

Karibuni sana kwenye banda la TIRA katika maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2024, tupate kujifunza, kushirikiana, na kujenga taifa lenye uelewa na utayari wa kutumia huduma za bima kwa manufaa ya wote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news