DODOMA-Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi (PDPC), Bw. Emmanuel Mkilia akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Zanzibar (PDPCZNZ), Bi. Rehema Abdallah wamekutana na kufanya mazungumzo na Kamishna wa Bima Tanzania Dkt. Baghayo Saqware katika ofisi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania leo tarehe Juni 14, 2024 jijini Dodoma.
Viongozi hao wamefanya mazungumzo kuhusu ushirikiano baina ya Taasisi hizo mbili na namna ambavyo TIRA inaweza kuboresha utendaji na utoaji huduma kwa ufanisi zaidi ikiwa na ulinzi Madhubuti wa taarifa binafsi.
Aidha, Bw. Mkilia yupo ziarani kukutana na Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma na Binafsi kuhimiza utekelezaji wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi hususani umuhimu wa kujisajili kwenye mfumo wa PDPC na kuteua Afisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwa kila taasisi ili kukidhi matakwa ya Sheria.
PDPC inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa Taasisi za Umma na Binafsi kupitia vyombo mbalimbali vya habari.