NA MWANAHAMISI MSANGI
TUME ya Madini Mkoa wa Songwe imeunda kikosi kazi maalum cha kupambana na kudhibiti utoroshaji wa madini na kusababisha serikali kukosa mapato.
Hayo yamesemwa na Afisa Madini Mkazi mkoani Songwe, Chone Malembo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwatembelea wachimbaji wadogo katika eneo la Mbangala lililopo mkoani humo.
“Kwa sasa kuna mawasiliano ambayo yanaendelea tunataka kutengeneza kikosi kazi madini Mkoa ambacho kazi yake itakuwa ni kufanya uchunguzi na kutoa taarifa kuhusu utoroshaji madini mahali husika ili kuchukua hatua stahiki lengo ni kudhibiti utoroshaji ambao husababisha Serikali kukosa mapato,”amesema Chone.