NA GODFREY NNKO
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya TEHAMA nchini (ICTC), Dkt. Nkundwe Moses Mwasaga amesema, hadi kufikia mwaka 2050 uchumi wa kidigitali utakuwa unaineemesha Tanzania zaidi.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya TEHAMA, Dkt. Nkundwe Mwasaga akichangia mada wakati wa Kongamano la Kwanza la Kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililofanyika Ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kongamano hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango limezinduliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango. (Picha kwa hisani ya Tume ya TEHAMA).
Dkt.Mwasaga ameyasema hayo Juni 8,2024 wakati akichangia mada katika Kongamano la Kwanza la Kitaifa kuhusu Maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 lililofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah uliopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
"Ningependa kuanza na takwimu ya miaka sifuri mpaka 35 ambayo inasema ni asilimia 37 ya populations yetu.
"Hii ina maana gani baada ya mwaka 2050, ina maana kwamba yule wa sifuri mwaka 2050 atakuwa na miaka 25 na watakuwa wana-interact na mifumo yote tunayoitumia.
"Ni watu wa kidigitali kabisa, yule wa 35 atakuwa na miaka 60, sasa ni wazi kwamba Tanzania ya mwaka 2050, itakuwa ni Tanzania ambayo ina demands kubwa ya vitu vya kidigitali.
"Tukiangalia takwimu za Afrika, TEHAMA inatoa mchango gani kwa uchumi mkubwa wa Afrika ni asilimia saba, sasa sisi tukifikia 2050 iwe saba au zaidi ya saba kwa sababu tuna namba na namba zinaonesha wazi namna ambavyo tunakuwa.
"Sasa hii dira inatakiwa ione huo uhitaji ambao unakuja ambao unahitajika kufanya hivyo."
Dkt.Mwasaga akizungumzia kuhusu namna ambavyo Tume ya TEHAMA imejipanga amesema, "sasa sisi tumejipanga vipi? Sisi tumejipanga kufanya mapinduzi ya kidigitali ambayo yanaangalia nguzo tano.
"Nguzo ya kwanza ni kuwapa watu ujuzi, pillar ya pili ni kuhakikisha hiyo mifumo inakuwa salama na inaweza kuaminika.
"Ya tatu, ni kuhakikisha watu wanapata huduma za mawasiliano bila ubaguzi, ya nne ni uchumi wa kidigitali na ya tano ni kuhakikisha masuala ya utafiti wa mambo ya kidijitali, ujasiriamali na ubunifu yanaangaliwa vizuri."
Mkurugenzi Mkuu huyo wa Tume ya TEHAMA amesema, katika uchumi wa kidigitali kuna vitu vikubwa vitatu ambavyo wanaviangalia ili kuhakikisha hayo mabadiliko yanaleta tija katika uchumi wetu.
"Cha kwanza ni kuhakikisha Watanzania mpaka mwaka kesho wanaanza kupata namba za kidigitali ambazo zitawasaidia kutumia mitandao vizuri.
"Pili, pia mifumo itakuwa inazungumza pamoja na kitu cha mwisho malipo yatakuwa yanafanyika kwa kutumia mifumo ya kidigitali.
"Na hii, ita-unlock ule uchumi ambao upo katika informal sector ambao mara nyingi ni ngumu kupata kodi kutoka kwao.
"Tumeangalia mara nyingi nchi mbalimbali mfano India, kwa kufanya hivyo makusanyo yameongezeka kuna nchi nyingine kama Kyrgyzstan na nyingine nyingi.
"Sasa, sisi tulipopimwa Tanzania kutoka kipimio cha Network Readiness Index ambacho kilifanyika Novemba mwaka jana tulionekana kwamba tunaonesha strength (nguvu) katika vitu tisa.
Ambapo ni vizuri tuangalie katika Dira ya 2050. Cha kwanza sheria zinazolinda faragha, hiyo ndiyo wanasema ni strength yetu.
Cha pili, ubora wa huduma za fibers zinazofika nyumbani kwa duniani wametu-rank namba 16, kuhusiana na Cyber Security duniani namba 45, kwa Afrika namba mbili.
Halafu kuna masuala ya machapisho ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence) namba 64 duniani halafu ukubwa wa soko letu la kidigitali Tanzania ukilipima duniani ni namba 68. Sasa hii inamaanisha nini?.
Kile nilichokisema kuhusu takwimu mwaka sifuri mpaka 35 ni kwamba ukubwa wa soko utaongezeka, na ukubwa wa soko ukiongezeka tunategemea viwanda vingi vya kutengeneza vifaa vya kompyuta na vitu vingine vitafunguliwa Tanzania kwa sababu namba tunazo.
"Tunavyozungumza sasa hivi, namba ya smartphone (simu janja) zipo milioni 20, sasa kumbuka wale wa 35 (miaka) watakapofika 60, hii namba itaongezeka na hii namba ikiongezeka hicho ni kivutio kimoja wapo cha kuhakikisha viwanda vinafunguliwa Tanzania ambavyo vinaweza kutengeneza hivyo vifaa.
"Na hii itafanya kitu kikubwa katika sekta hii ya TEHAMA. Cha kwanza ni kutengeneza kazi kwa vijana ambao wapo wengi, cha pili ni kuhakikisha sekta hii inatoa mchango mkubwa katika pato kuu la Serikali,"amefafanua kwa kina Dkt.Mwasaga.