Tunaweza Mongolandege Ukonga wakabidhiwa Katiba,atoa neno kwa Rais Dkt.Samia

DAR-Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mongolandege, Rajabu Tego amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango kwa kutoa miongozo yenye unafuu katika usajili wa vikundi mbalimbali kisheria.Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mongolandege, Jimbo la Ukonga jijini Dar ea Salaam, Rajabu Tego akikabidhi katiba kwa mwanachama wa kikundi cha Tunaweza leo Juni 16, 2024.

Hayo ameyasema leo Juni 16, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi katiba, kanuni na kadi ya mwanachama wa kikundi cha Tunaweza ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanachama wa kikundi cha Tunaweza wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo.

Tego amesema kuwa kuanzishwa kwa miongozo hiyo kumerahisisha usajili wa vikundi na kuondoa dhana ya kudhulimiana kutokana na fedha kukaa mifukoni mwa viongozi.

“Ni jambo la kumpongeza Rais Samia kuanzisha miongozo hiyo kwa vikundi vya kijamii, lakini nakipongeza kikundi cha Tunaweza ambacho kimepata usajili hivyo hata michango wanayotoa itakuwa mahala salama na kuwezesha kikundi kupata maendeleo na hata kwa mwanachama mmoja mmoja pindi inapotolewa mikopo,” amesema.
Mwenyekiti wa kikundi cha Tunaweza, Dk Abdallah Mandai (katikati) akizungumza wakati wa kukabidhi katiba kwà wanachama, kulia ni Katibu wa kikundi hicho cha Tunaweza, Gervas Paulo, na kushoto ni katibu msaidizi Ramadhan Mtuli.

Naye Katibu wa kikundi hicho cha Tunaweza, Gervas Paulo, amesema kuwa kikundi hicho kina wanachama 118 ambapo kilianzishwa Machi 8, 2023.
“Kikundi cha Tunaweza tayari kimepata usajili, na leo tumegawa katiba kwa wanachama ili kila mmoja afahamu sheria na kanuni tulizojiwekea ili kuepuka kwenda kinyume na taratibu za makubaliano yetu,” amesema.
Katibu huyo amesema kuwa kikundi hiki kimeanzishwa kwa nia ya kusaidiana katika nyanja mbalimbali lakini pia katika kutoa misaada kwa watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

“Tunashirikiana katika makundi hayo na wanachama wamekuwa wakichangia ada ya sh.5,000 kwa kila mwezi na kuhifadhiwa benki ingawa bado kuna baadhi ya wanachama wako nyuma katika uchangiaji jambo ambalo wanakwenda kinyume na katiba yetu,” amesema.
Ameongeza kuwa,kuna mafanikio mbalimbali ambayo yamepatikana lakini pia kuna changamoto ya kuwepo kwa baadhi ya wanachama ambao si waaminifu wenye mtazamo hasi wa kuomba kupata matatizo ili wapate fedha tu hivyo tunashauri ni vyema wote tukawa wazalendo.

Naye Katibu msaidizi Ramadhan Mtuli amesema kuwa, kikundi cha Tunaweza kinapokea wanachama kutoka maeneo mbalimbali ili mradi mwanachama awe na akili timamu.

“Tunapokea wanachama kutoka maeneo mbalimbali ili mradi awe na akili timamu hivyo tunawakaribisha wenye nia ya kutaka kujiunga na Tunaweza kwani ni kikundi kilichosajiliwa kisheria,” amesema.
Hata hivyo,amempongeza Rais Samia kwa kazi nzuri na kubwa anazozifanya hivyo rai yao kwake ni kuomba kuwafikia katika utaratibu wa utoaji mikopo ili wanachama waweze kunufaika na kupata maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news