GEITA-Waziri Mkuu Kassim Majakiwa amesema Serikali inaendelea kujikita katika kuhakikisha inaimarisha na kuwashirikisha wavuvi na wafugaji katika mipango ya maendeleo.

Amesema kuwa, mradi huo unaotoa fursa kwa yeyote aliyeanza na anayetaka kujikita kwenye sekta ya uvuvi kunufaika na kujiingizia kipato. “Kitendo cha Serikali kuleta soko hili hapa ni kuhakikisha wanasogeza fursa kwa wavuvi wa eneo hili, soko hilo ni lenu, imarisheni uchumi wenu kupitia soko hili.”
Ameongeza soko hilo litakuwa na uwezo wa kukausha hadi tani 10 za dagaa kwa siku kwa kuwa kutawekwa mtambo wa kukausha samaki.
“Tutaweka mafriji makubwa mawili ya kutunzia samaki, pamoja na chumba maalum cha kuzalisha barafu.”
