Tuyaenzi mema yote yaliyofanywa na Tixon Nzunda-Waziri Mkuu

DAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali na Watanzania wataendelea kumkumbuka na kuyaenzi mema yote yaliyoyafanywa na aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, marehemu Tixon Nzunda.Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo Ijumaa, Juni 21, 2024 alipokwenda kuhani msiba wa marehemu Nzunda, nyumbani kwa marehemu Goba, Dar es Salaam. Marehemu Nzunda alifariki Juni 18, mwaka huu kwa ajali ya gari.
“...Tunajukumu la la kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ili ailaze roho ya marehemu Nzunda pahala pema, pia tunajukumu la kuipa faraja familia yake.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa uwezo aliokuwa nao Marehemu Nzunda ulikuwa wa aina yake na ni pigo kutokana na kazi kubwa aliyokuwa akiifanya.

Amesema kuwa vijana wengi walijifunza kutoka kwake. “Sisi tunamengi ya kusema kama ushuhuda wa yale aliyoyafanya katika kipindi chote cha uongozi wake.”
Awali, mtoto wa marehemu, Victor Nzunda alisema marehemu baba yao aliwaasa waishi maisha ya kufanya ibada. “Baba yetu alikuwa mcha Mungu.”

Victor alisema baba yao alikuwa akiwaunganisha watu wenye mahitaji wakiwemo yatima na wazee pamoja kwenda hospitali kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news