Ujenzi ofisi za Wizara ya Madini Mtumba wafikia asilimia 82

DODOMA-Ujenzi wa Jengo la ofisi ya Wizara ya Madini katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma umefikia asilimia 82 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2024.
Hayo yamebainishwa Juni 4, 2034 na Meneja wa mradi huo, Mhandisi Peter Mwaisabula kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambaye ni Mkandarasi wakati akielezea maendeleo ya mradi mbele ya Menejimenti ya Wizara ya Madini iliyomtembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Madini, Festus Mbwilo amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa mradi huo kwa wakati.
Aidha, Mbwilo amemtaka mkandarasi kutosita kuwasiliana na Wizara pale wanapokumbana na changamoto yeyote ili kuondoa vikwazo vinavyoweza kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news