Undeni vikundi ili mnufaike na mikopo-Waziri Mkuu

GEITA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 2, 2024 amezindua jengo la kituo cha uwezeshaji wananchi kiuchumi katika halmashauri ya wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita.
Jengo hilo ambalo limejengwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakazi wa eneo hilo kutumia fursa hiyo kupata elimu ya biashara na ujasiriamali pamoja na mikopo ili wajiendeleze kiuchumi.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wananchi hao kuunda vikundi ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali.

“Vikundi vinakopesheka kwa urahisi hata anuani yake ni rahisi pia”.
Kwa Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Ummy Nderiananga amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwenye Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ambayo imewawezesha kutekeleza programu mbalimbali za uwezeshaji wananchi kiuchumi.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu tutaendelea kulisimamia Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) ili liweze kufanya vizuri katika uwezeshaji wananchi kiuchumi.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news