Utakayojifunza ukifika banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ndani ya Maonesho ya Sabasaba

DAR-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inashiriki Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni 2023 hadi 14 Julai 2024.
Katika Maonesho hayo BoT inatoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ambapo wananchi wanapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo sera za fedha.

Pia, namna yakuwekeza katika dhamana za serikali, mifumo ya malipo ya taifa, namna BoT inasimamia sekta ya fedha nchini, utatuzi wa malalamiko ya mtumiaji wa huduma za kifedha.
Vile vile,masuala ya ajira na utumishi Benki Kuu, nafasi za masomo katika Chuo cha BoT pamoja na Bodi ya Bima ya Amana.

Aidha, BoT inatoa elimu kuhusu utambuzi wa alama za usalama katika noti zetu na njia sahihi za utunzaji wa noti na sarafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news