DODOMA-"Gharama za kuunganisha umeme maeneo ya vijijini katika njia moja ni shilingi 27,000 na mijini shilingi 320,960 kwa kipindi cha nyuma kwa miradi ya vijijini yaani REA ilikuwa inatoza shilingi 27,000 na TANESCO shilingi 177,000.
"Kutokana na malalamiko ya wananchi ya bei tofauti kati ya REA na TANESCO ya kuunganishwa umeme vijijini, Serikali iliiamuru TANESCO kushusha bei na kuwa shilingi 27,000 kama REA na tofauti ililipwa na Serikali,"Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Judith Kapinga katika Mkutano wa 25 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.