DODOMA-Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Judith Kapinga amesema,wastani wa magari 1,159 yaliwekewa mfumo wa kutumia gesi mwaka 2021 huku idadi ya magari ya kutumia gesi ikiendelea kuongezeka ambapo kwa mwaka 2022/23 yamefikia 5,100.
"Aidha, karakana za kubadilisha mfumo wa magari ili kutumia gesi zimeongezeka kutoka karakana moja ya DIT hadi nane,"Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri Nishati Bungeni Dodoma Juni 12, 2024.