SINGIDA-Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida unahudumia jumla ya kilomita 1,718.31 za Barabara Kuu na Barabara za Mkoa.
Kati ya hizo, kilomita 490.30 ni barabara za lami sawa na asilimia 28.5 na sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilomita 1,228.01 ni barabara za changarawe sawa na asilimia 71.5.
Hali ya barabara katika Mkoa wa Singida inaridhisha, ambapo asilimia 80.0 zina hali nzuri, asilimia 15.3 wastani na asilimia 4.7 zina hali mbaya.
Katika kipindi cha miaka mitatu madarakani ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameipatia TANROADS takribani shilingi bilioni 93 kwa ajili ya miradi ya uwekaji taa za barabarani,ujenzi na matengenezo ya barabara pamoja na ujenzi wa madaraja.