VIDEO:Waziri Mkuu aiagiza DCEA kuendelea kufanya operesheni dhidi ya dawa za kulevya kote nchini

MWANZA-Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) kuendelea kufanya operesheni dhidi ya dawa za kulevya kwenye maeneo yote nchini.
Pichani ni moja kati ya operesheni iliyofanywa Mei 31,2023 na DCEA ikiongozwa na Kamishna Jenerali,Aretas Lyimo ambapo ilifanikiwa kukamata gunia 482 za bangi iliyokuwa tayari kusafirishwa kwenye masoko na kuteketeza jumla ya hekari 101 za mashamba ya bangi yaliyokadiriwa kuwa na bangi mbichi gunia 550 katika eneo la Kisimiri Juu hulo Kata ya Uwalu, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.Tazama video chini;
Ametoa agizo hilo leo Juni 30, 2024 wakati akizungumza na wananchi na wadau mbalimbali walioshiriki kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Nyamagana, jijini Mwanza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news