NA EVA NGOWI
WF
SERIKALI imewashauri wananchi kusajili vikundi vyao vya huduma ndogo za fedha kupitia mfumo wa Wezesha Portal ambayo ni njia rahisi na haina gharama yoyote.
Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Omar Bakari, akitoa elimu ya fedha, uwekezaji na utaratibu wa kujiunga na vikundi kwa wanakijiji wa Kipeta (hawamo pichani) iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Omar Bakari, wakati akitoa Elimu ya Huduma Ndogo za Fedha katika Kijiji cha Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Afisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Uendeshaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw. Salim Kimaro (kulia), akimkabidhi Mjasiriamali mdogo, Bw.Juma Hassan, zawadi ya fulana wakati wa utoaji elimu ya fedha iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Mratibu wa Huduma Ndogo za Fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, Bw. Winfred Mwamkalaba (kushoto), akimkabidhi mjasiriamali mdogo, Bw. George Kajala, zawadi ya fulana wakati wa utoaji elimu ya fedha iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Bw. Bakari alisema kuwa kabla ya kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha ni vyema wananchi wanaotaka kuanzisha vikundi hivyo wakajiridhisha kuhusu wanachama wao wanaotaka kujiunga nao ili kuepukana na lawama na baadhi ya wajumbe kukimbia familia zao kutokana na madeni.
“Kabla ya kujiunga kwenye kikundi kitu cha kwanza lazima wawe wanatoka eneo moja ili kurahisisha utambuzi katika Serikali za mitaa, pili lazima waaminiane, tatu wawe na lengo moja lililosababisha wao waamue kuanzisha kikundi,"amesema Bw. Bakari.
Afisa Uwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Bw. Omar Bakari, akitoa elimu ya usajili wa vikundi vya huduma ndogo za fedha iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Baadhi ya Wanavikundi na Wajasiriamali wadogo wadogo wakisikiliza elimu ya fedha, uwekezaji na utaratibu wa kujiunga na vikundi iliyofanyika katika moja ya darasa la Shule ya Msingi Kipeta, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, mkoani Rukwa.
Aidha, Bw. Bakari aliwawashawishi wananchi kuendelea kusajili vikundi vyao kupitia wezesha Portal kwani inaokoa muda.
Wezesha Portal ni jukwaa la dijitali lililoundwa kusaidia wajasiriamali na wafanyabiashara katika kukuza biashara zao, kupata mafunzo, na kupata rasilimali zingine za kuwasaidia kibiashara.