Viongozi wajifunze kusikiliza na kuzifanyia kazi changamoto za wananchi-Mwinjilisti Temba

DAR-Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amewataka viongozi wa kiafrika ambao wanapewa nafasi ya kuwatumikia wananchi kuwa na tabia ya kusikiliza.Pia,kuzifanyia kazi changamoto zao kwa wakati ili kuepuka misuguano ambayo mara nyingi imekuwa kikwazo na uharibifu wa mali za umma.
Temba ameyasema hayo wakati akirejea unabii alioutoa Agosti,2022 jijini Nairobi nchini Kenya kuhusu umuhimu wa viongozi kuwa wasikivu na watatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi.Soma kwa kina hapa》》》

Amesema, wakati akiwa nchini humo ikiwa ni katika hatua za maandalizi ya uchaguzi ambao ulimuweka madarakani, Dkt.William Ruto alisema, atapata ushindi, lakini akishindwa kuyatimiza au kuyafanyia kazi mahitaji ya wananchi, uongozi wake utapitia katika misukosuko.

"Mheshimiwa Ruto anaweza kushinda Urais, lakini ushindi wake unaweza kuwa wa furaha kipindi cha awali, kadri siku zitakaposonga mbele uongozi wake utageuka kuwa tanuru la moto, ninaona linaweza kuibuka vuguvugu la vijana ambao watakuwa hawakubaliani na namna ambavyo hali ya kiuchumi itakavyokuwa,"alisisitiza Mwinjilisti Temba akiwa Nairobi mwezi Agosti,2022.

Mwinjilisti Temba amefafanua kuwa,uongozi ambao hautakuwa na malumbano ni ule ambao viongozi walioaminiwa watatekeleza ahadi na majukumu yao kwa manufaa ya umma.

"Viongozi wengi barani Afrika wamekuwa wakituhumiwa mara kwa mara kujinufaisha wenyewe kupitia rasilimali za umma. Hali hiyo hata kama ina ukweli imekuwa ikichangia raia kuwa na hasira za mara kwa mara.

"Kikubwa kila mmoja ajitathimini na kutenda yale aliyoahidi kwa uaminifu, kusimamia rasilimali za umma ili ziweze kunufaisha watu wote, na pale inapobainika kuna miongoni mwa hao viongozi anakwenda kinyume, basi awajibishwe ili umma uone kuwa, kila jambo linatendeka kwa haki na usawa."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news