Vituo 16 vya MAT vilivyopo nchini, ripoti wafanyabiashara wa dawa za kulevya bure simu 119

VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MEDICALLY ASSISTED THERAPY-MAT)

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), vituo hivi husimamiwa na Serikali na huhudumia waathirika wa dawa ya kulevya aina ya afyuni kama vile heroin na baadhi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya.

Waathirika wanaotibiwa kwenye vituo hivi hutibiwa kwa kutumia dawa mfano Methadone.

Aidha,waathirika wanatakiwa kuhudhuria matibabu kila siku mpaka watakapomaliza matibabu. Huduma ya MAT hutolewa bure chini ya uangalizi wa wataalamu.

HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MAT)

1.Kupatiwa dawa aina ya methadone
2.Kupatiwa Elimu juu ya UKIMWI na Kupima VVU
3.Kupatiwa dawa za kufubaza VVU (Antiretroviral therapy)
4.Kupatiwa elimu ya Kinga, Kupima na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Kifua kikuu.
5.Kupatiwa elimu ya Kinga na kutibu Magonjwa ya zinaa
6.Kupatiwa Ushauri nasaha
7.Kupatiwa matibabu ya magonjwa ya Akili
8.Kupatiwa Elimu juu ya maambukizi ya Homa ya ini B na C.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news