Wadau wa madini wapigwa msasa Dodoma

DODOMA-Tume ya Madini inaendelea kutoa elimu kwa wadau wa madini na wananchi wote kutoka katika Mkoa wa Dodoma kwenye Wiki ya Maonesho ya Madini inayoambatana na Kongamano la Wachimbaji wa Madini yanayoendelea katika Viwanja vya Jakaya Kikwete leo Juni 22, 2024 jijini Dodoma.Elimu inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini, taratibu za upatikanaji wa leseni za madini nchini, biashara ya madini na taratibu za usalama wa afya na mazingira kwenye migodi ya madini.
Maeneo mengine ni pamoja na namna watanzania wanaweza kushiriki katika Sekta ya Madini kupitia utoaji wa huduma mbalimbali kwenye migodi ya madini na mchango wa kampuni za uchimbaji wa madini kwenye jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news